Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 07:58

Chama tawala chatarajiwa kupata ushindi Angola

Joao Lourenco, akionyesha kidole chake chenye rangi ya wino akikabiliana na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika uchaguzi huko Luanda, Angola, Agosti 25, 2017. Mgombea huyo anaongoza katika uchaguzi wa sasa akitarajiwa kushinda muhula wa pili. (AP Photo/Bruno Fonseca.

Chama tawala nchini Angola kinatarajiwa kuongeza muda wake utawala kwa miaka mingine mitano, na kuikipa takriban jumla ya miaka 52 madarakani. Chama kikuu cha upinzani kilisema huenda kitawasilisha changamoto kwa matokeo ya upigaji kura wa Jumamosi.

Rais aliyepo madarakani Joao Lourenco wa chama cha People’s Movement for the Liberation of Angola kinachojulikana kama MPLA, ameshinda muhula mwingine wa miaka mitano badarakani baada ya kupata 51% ya kura katika uchaguzi wa rais Jumatano huku ikiwa kura zaidi ya 97% zikiwa zimehesabiwa.

Mpinzani mkuu wa Lourenco, Adalberto Costa Jr. wa National Union for the Liberation of Angola, UNITA, alipata 44% ya kura. Katika uchaguzi wa mwisho mwaka 2017, UNITA ilipata 26% ya kura za urais.

Chama tawala kimeshinda viti 124 vya bunge kati ya 220 viliyokuwa vinagombaniwa.

Kundi kuu la upinzani limehoji uwazi wa tume ya uchaguzi kwa matokeo ya urais na bado halijakubali matokeo ya kura ya Jumatano.

Umaarufu wa chama tawala katika uchaguzi huu umeshuka kwa pointi 10 za asilimia kutoka uchaguzi uliopita wakati walipokuwa katika 61% ya kura zilizopigwa.

Kampeni za uchaguzi wa tano wa Angola zililenga kwenye masuala ya uchumi na umaskini, huku wapiga kura wengi wakilalamika kuwa wanasiasa wamewaacha, licha ya nchi kuwa na rasilimali ya mafuta.

XS
SM
MD
LG