Chama cha kati kulia cha National Coalition kimetangaza ushindi Jumapili baada ya kuhesabiwa kwa takriban asilimia 97.7 ya kura zilizopigwa, kikiongoza kwa asilimia 20.7. Chama cha The Finns chenye msimamo wa kulia kilifuata kwa asilimia 20.1 huku kile cha Social Democrats kishikilia nafasi ya tatu kwa asilimia 19.9.
Kutokana na vyama vyote kujipatia takriban asilimia 20 ya kura zilizopigwa, hakuna chenye uwezo wa kuunda serikali peke yake. Zaidi ya wagombea 2,400 kutoka vyama 22 waliwania kupata nafasi kwenye bunge la Nordic lenye jumla ya viti 200. Marin mwenye umri wa miaka 37 ni miongoni mwa viongozi wachanga zaidi barani Ulaya, wakati akisifika kutokana na namna yeye na serikali yake walivyoshughulikia janga la Covid-19. Pia amepata sifa kubwa akiwa na Rais Sauli Niinistokwa kushinikiza ombi lililokubaliwa la Finland kujiunga na NATO.