Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 20, 2025 Local time: 12:47

Tanzania: CHADEMA, chaitisha maandamano ya amani kupinga marekebisho ya sheria ya Uchaguzi


Wafuasi wa Chadema wakishangilia baada ya marufuku ya kutokutana kuondolewa 2016. Picha ya maktaba.
Wafuasi wa Chadema wakishangilia baada ya marufuku ya kutokutana kuondolewa 2016. Picha ya maktaba.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimetangaza maandamano ya amani nchi nzima kupinga mswaada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wameitaka serikali kusimamia kikamilifu sera ya maridhiano ili kuepusha migogoro ya kisiasa inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Hayo yamesemwa baada ya chama hicho cha upinzani kuelezea kutokuridhishwa na mchakato wa ukusanyaji wa maoni juu ya mswaada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi na hivyo kufanya maamuzi ya kutangaza maandamano ya amani ya nchi nzima kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuuondoa mswaada huo bungeni.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema licha ya kuwepo kwa jitihada kubwa za kuleta maridhiano ya kidemokrasia kupitia sera ya maridhiano ya Rais Samia Suluhu Hassan, sera hiyo imeshindwa kutoa matumaini kwa vyama vya upinzani. Dkt Paul Loisulie mchambuzi wa siasa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma anasema sera hiyo imepoteza matumaini kwa vyama vya upinzani baada ya kuonekana mapungufu katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni juu ya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi na ndio sababu ya chama hicho kuitisha maandamano.

Forum

XS
SM
MD
LG