Utawala wa kijeshi umeitisha kura hiyo ikiwa kama hatua muhimu kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao ambao uliahidiwa kwa muda mrefu kurejesha utawala wa kidemokrasia baada ya kukamata madaraka mwaka 2021 kufutaia kuuwawa kwa rais Idriss Deby, wakati akiwa kwenye uwanja wa mapambano wakati wa mzozo na waasi.
Moja wapo ya mapendekezo kwenye katiba mpya ni kuundwa kwa jumuiya zenye utawala kiasi, zikiwa na mabunge ya kieneo na mabaraza ya viongozi wa kitamaduni. Hata hivyo baadhi ya vyama vya upinzani na makundi ya waasi wametaka "hapana" kwa kura hiyo au watasusia zoezi hilo.
Forum