Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:32

Castro: Uhusiano kamili kati ya Marekani na Cuba hautatokea


Rais wa Cuba, Raul Castro akiwasili kwenye kikao cha 70 kwenye mkutano wa baraza kuu la UN huko New York, Sept. 28, 2015.
Rais wa Cuba, Raul Castro akiwasili kwenye kikao cha 70 kwenye mkutano wa baraza kuu la UN huko New York, Sept. 28, 2015.

Uhusiano kamili wa kawaida kati ya Marekani na Cuba hauwezi kutokea anasema kiongozi wa Cuba, Raul Castro, hadi Marekani iondoe marufuku ya biashara, imalize kazi zake zisizo halali kwenye kituo cha jeshi cha Guantanamo Bay, iache matangazo yanayoleta hali ya ukosefu wa uthabiti kwa Cuba na kuwalipa fidia wa-Cuba kwa uharibifu wa kiuchumi.

Katika hotuba yake ya kwanza kuwahi kutolewa kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Castro alisema serikali yake itaendelea kuwasilisha rasimu ya azimio dhidi ya marufuku ya biashara ya Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa marufuku hiyo bado vipo.

Rais wa Marekani Barack Obama aliunga mkono kwa kuondolewa marufuku, utaratibu ambao unahitaji hatua za bunge.

Rais Barack Obama kwenye mkutano wa UN mjini New York
Rais Barack Obama kwenye mkutano wa UN mjini New York

Mapema Jumatatu Rais Barack Obama aliuambia Umoja wa Mataifa kwamba wakati Marekani inaendelea kuwa na tofauti na Cuba juu ya masuala kama vile haki za binadamu, tofauti hizi hivi sasa zitazungumziwa kupitia njia ambazo zinajumuisha uhusiano wa kidiplomasia.

“Mabadiliko hayawezi kutokea usiku mmoja kwa Cuba”, alisema bwana Obama. Bwana Obama alisema ana Imani kwamba “uwazi, sio vitisho” huwenda vitasaidia “mageuzi na maisha bora wanayostahili watu wa Cuba”.

Rais Obama alipigiwa makofi pale aliposema alikuwa na imani kwamba bunge hatimaye litaondoa marufuku ya biashara.

Rais Raul Castro wa Cuba (L) na Rais Barack Obama
Rais Raul Castro wa Cuba (L) na Rais Barack Obama

Rais Obama na Rais Castro wanatarajiwa kukutana pembeni ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, mkutano wao wa pili kwa mwaka huu.

Viongozi hao wawili walikutana kwa mazungumzo mwezi April katika mkutano wa Americas huko Panama.

XS
SM
MD
LG