Mgogoro wa mwezi Desemba kati ya wafugaji na wavuvi ulisababisha vifo vya takriban watu 40 na kuwasukuma zaidi ya 100,000 nchini Chad. Wengi wamerejea lakini makundi ya misaada yanasema waliokimbia makazi yao wanapata shida kuishi.
Mfanyakazi wa misaada katika hospitali ya serikali ya Cameroon huko Maroua anamwambia mama mmoja kwamba mtoto wake bado ana utapiamlo uliokithiri, na maisha yake yanaweza kuwa hatarini ikiwa mama yake atamtoa mtoto huyo hospitali.
Ombi la mfanyakazi huyo wa misaada lilitangazwa mara kadhaa Jumatatu kwenye vyombo vya habari vya ndani ikiwa ni pamoja na shirika la utangazaji la umma la Cameroon- CRTV.
Hatimaye mama anakubali kubaki hospitali na mwanawe.
Maroua ni mji mkuu wa eneo la Kaskazini la Mbali la Cameroon ambalo linashirikiana mpaka na Nigeria na Chad. Serikali ya Cameroon inasema maelfu ya watu katika mpaka wa kaskazini na Chad na Nigeria wanakabiliwa na utapiamlo huku watoto wengi wakifariki dunia katika wiki chache zilizopita.
Mchuuzi wa nyanya Mota Nyako mwenye umri wa miaka 28 anasema ana bahati mwanawe mwenye utapiamlo hakufa.
Anasema alimkimbiza mtoto wake wa miaka 2 hospitalini kwa sababu alikuwa akitapika bila kukoma na alikuwa anahaisha sana. Anasema mwanawe ameanza kunenepa baada ya kupata matibabu katika hospitali hiyo kwa muda wa wiki moja. Nyako anasema atakwenda kuwajulisha wanawake ambao watoto wao wanapungua uzito ili kuwaleta mara moja hospitali ambapo maisha yao yataokolewa.
Nyako, ambaye alizungumza kupitia programu ya whatsapp kutoka Maroua, alisema alikimbia kutoka wilaya ya mpakani na Chad, wakati wa mapigano na wakulima na wavuvi kuhusu maji. Nyako alisema yeye ni maskini na hawezi kumudu chakula cha kutosha yeye na mwanawe.
Wizara ya Afya ya Umma ya Cameroon inasema maelfu ya watu wapya wenye utapiamlo walioripotiwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita wanaongeza zaidi ya watoto 100,000 kaskazini mwa Cameroon ambao kwa sasa wanaugua utapiamlo mkali.
Flobert Danbe ni afisa wa afya wa Cameroon anayehusika na utapiamlo katika eneo la Kaskazini la Mbali la Cameroon.
Cameroon inasema maelfu ya raia wake walikimbia migogoro ya umwagaji damu Desemba 2021 kuhusu mivutanoya kupata maji kati ya wafugaji na wavuvi hadi Mayo Tsanaga.
Baadhi ya watu waliokimbia makazi yao wamerejea lakini mashamba yao yameharibiwa vibaya na vita au mvua kubwa na mafuriko.