Majarbio mawili kutoka chama kilichopata ushindi cha Move Forward cha kutaka kiongozi wake Pita Limjaroerat kuidhinishwa kama waziri mkuu yamepingwa na wajumbe wa kikonsavative pamoja na wale kutoka jeshini.
Chama cha Pheu Thai kilichopata nafasi ya pili na ambacho ni sehemu ya muungano wa vyama 8 kinatarajiwa kupendekeza kiongozi atakayechukua nafasi ya waziri mkuu.
Wapiga kura wa taifa hilo la pili kiuchumi kusini mashariki mwa Asia walipatia chama cha Move Forward ushindi usiotarajiwa, dhidi ya wapinzani waliokuwa wakifadhiliwa na jeshi, ambalo limekuwa likiendesha siasa kwa karibu muongo mmoja nchini humo.
Forum