Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 10:09

Bunge la Marekani linapiga kura juu ya mpango wa kuisaidia Israel dola bilioni 14.3


Baraza la Wawakilishi la Marekani katika moja ya michakato yake ya upigaji kura
Baraza la Wawakilishi la Marekani katika moja ya michakato yake ya upigaji kura

Wa-Republican walizindua mswaada huo Jumatatu, katika hatua ya kwanza kubwa ya kisheria chini ya Spika mpya Mike Johnson, licha ya ombi la Rais Joe Biden la ufadhili mpana wa dola bilioni 106 ikiwa ni pamoja na msaada kwa Israeli, Taiwan na Ukraine, pamoja na misaada ya kibinadamu

Baraza la Wawakilishi la Marekani linapanga kupiga kura leo Alhamisi juu ya mpango wa Republican wa kuipatia Israel msaada wa dola bilioni 14.3 kwa kupunguza ufadhili kwa Internal Revenue Service (IRS), na kuanzisha malumbano na Seneti inayodhibitiwa na wademocratic pamoja na White House.

Wa-Republican walizindua mswaada huo Jumatatu, katika hatua ya kwanza kubwa ya kisheria chini ya Spika mpya Mike Johnson, licha ya ombi la Rais Joe Biden la ufadhili mpana wa dola bilioni 106 ikiwa ni pamoja na msaada kwa Israeli, Taiwan na Ukraine, pamoja na misaada ya kibinadamu.

Mswaada huo utakabiliwa na mtihani wake wa kwanza wa uungaji mkono katika utaratibu wa upigaji kura saa za asubuhi, kikwazo ambacho kinahitaji kurekebishwa kabla ya upigaji kura wmwisho juu ya kifungu hicho baadaye mchana.

Wa-Republican wana wingi wa viti 221 kwa 212 katika baraza la wawakilishi, lakini chama cha Democratic cha Biden kinadhibiti baraza la seneti kwa kura 51-49. Ili kuwa sheria, mswaada huo utalazimika kupitishwa na Baraza la Wawakilishi na Seneti na kisha kutiwa saini na Biden.

Seneta wa ngazi ya juu Chuck Schumer amesema mswaada huo wa Republican hautashughulikiwa utakapowasili katika baraza la seneti hatua ya juu hathataa kama utapitishwa na bunge. White House imetishia kutumia kura ya turufu.

wademocrats walipinga kupunguza fedha kwa ajili ya IRS, wakisema itaongeza nakisi ya bajeti ya nchi kwa kupunguza ukusanyaji wa kodi.

Pia wamesema ni muhimu kuendelea kuiunga mkono Ukraine wakati ikipambana na uvamizi wa Russia ulioanza Februari mwaka 2022.

Wakati wa-Democrat na wa-Republican wengi bado wanaiunga mkono Ukraine, kundi dogo lenye sauti kali la wa-Republican wanahoji kutuma fedha zaidi kwa serikali huko Kyiv wakati kuna nakisi kubwa katika bajeti.

Forum

XS
SM
MD
LG