Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:25

Brazil, Mexico kuchuana raundi ya pili


Thiago Silva, kushoto, na Neymar baada ya kufunga goli la pili la Brazil, 27 juni 2018.
Thiago Silva, kushoto, na Neymar baada ya kufunga goli la pili la Brazil, 27 juni 2018.

Brazil na Mexico, timu zinazojuana sana katika ukanda wa Amerika Kusini, zitaongeza utamu wa kombe la dunia zitakapokutana katika raundi ya pili ya mtoano wa fainali za Russia 2018.

Brazil ilifanikiwa kuingia raundi ya pili kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia Jumatano wakati Mexico walitoka katika kundi F katika nafasi ya pili ingawa walichapwa 3-0na Sweden.

Sweden watacheza na Switzerland katika raundi ya pili baada ya Waswiss kuchopoka katika kundi E nyuma ya Brazil baada ya kutoka sare 2-2 na Costa Rica.

Golikipa wa Serbia Vladimir Stojković amnyima Neymar fursa ya kupata goli katika mechi yao ya Jumatano.
Golikipa wa Serbia Vladimir Stojković amnyima Neymar fursa ya kupata goli katika mechi yao ya Jumatano.

​Mechi sita za raundi ya pili ambazo zitachezwa kati ya Jumamosi June 30 na Jumanne July 3 zimekwishapangika sasa, nazo ni:

Uruguay na Ureno; Ufaransa na Argentina; Spain na Russia; Croatia na Denmark; Brazil na Mexico; Switzerland na Sweden.

Makundi ya G na H yanamaliza mechi za makundi Alhamisi. Uingereza na Belgium, zote zikiwa na pointi sita kila moja zimekwishaingia raundi ya pili. Zinakutana kuamua nani atakuwa wa kwanza na wa pili katika kundi hilo. Tunisia na Panama zinakutana kujaribu kumaliza mashindano angalau na pointi moja.

Katika kundi H, Senegal - timu pekee ya Afrika iliyobaki katika mashindano hayo - itachuana na timu kali ya Colombia lakini ikipata sare tu itafanikiwa kuingia raundi ya pili. Japan nayo inahitaji sare tu dhidi ya Poland kuingia raundi ya pili.

XS
SM
MD
LG