Nchi ya Botswana ina kiwango cha juu kilichoripotiwa na kinachoongezeka cha visa vya ubakaji. Wabunge nchini humo hivi karibuni waliunda kamati ya kushughulikia shida hiyo na kupanga kuanzisha usajili wa wahalifu wa kingono.
Lakini wanaharakati kama mwathirika wa ubakaji Refilwe Mooki wanasema hatua hizo hazitoshi.
Mwimbaji na mwanaharakati Refilwe Mooki alichukua masomo ya kujilinda baada ya kubakwa mwaka 2017.
Mwaka jana, jeraha lake la moyoni lilifunguliwa tena wakati dada yake mdogo pia aliposhambuliwa.
Mooki anaongoza kampeni ya Sema Hapana kwa ubakaji nchini Botswana, ambapo visa vya ubakaji vilivyoripotiwa vimeongezeka katika miaka michache iliyopita.
Serikali imegundua kuwa masharti ya janga la corona yameongeza unyanyasaji wa kijinsia, na mwaka huu ilitangaza kamati na daftari la usajili wa makosa ya kijinsia kushughulikia shida hiyo.
Lakini wanaharakati kama Desmond Lunga wanasema wanahitaji hatua zaidi ya sera wanahitaji hatua.
Wahanga wa ubakaji nchini Botswana wanasema polisi hawachukui shida zao kwa uzito unaostahili, na kesi mara nyingi hazifikishwi mahakamani.
Ili kushughulikia shida hizo, mamlaka zinasema zinajaribu vitengo vya unyanyasaji wa kijinsia katika vituo vya polisi na mahakama maalum ili kuharakisha kesi zao.
Hiyo inaongeza matumaini kwamba sauti za waathirika kama Mooki mwishowe zinaweza kusikika.