Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:16

Boakai aapishwa rasmi kuiongoza Liberia


Rais Joseph Boakai wa Liberia akihutubia mara baada ya kula kiapo mjini Monrovia. Jan. 22, 2024.
Rais Joseph Boakai wa Liberia akihutubia mara baada ya kula kiapo mjini Monrovia. Jan. 22, 2024.

Boakai alimshinda Weah katika uchaguzi wa marudio wa Novemba kwa asilimia 50.64 ya kura dhidi ya asilimia 49.36.

Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai ameahidi kupambana na ufisadi katika taifa hilo la Afrika Magharibi wakati alipoapishwa Jumatatu kushika madaraka kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi dhidi ya nyota wa zamani wa soka George Weah.

Boakai mwenye umri wa miaka 79 alimshinda Weah kwa kiwango kidogo katika uchaguzi wa marudio wa Novemba, kwa asilimia 50.64 ya kura dhidi ya asilimia 49.36. “Tunashuhudia nyakati ngumu, tunaona kutokufaulu. "Tunaona ufisadi katika maeneo ya juu na ya chini. Na-ni katika hali hizi na zinazoendana ambapo tumekuja kuwaokoa,” Boakai alitangaza katika sherehe yake ya kuapishwa.

Boakai ambaye umri wake na afya yake ndio chanzo cha majadiliano mengi nchini humo, alilazimika kupumzika na kukaa chini ili kumaliza hotuba yake kutokana na hali ya joto kali.

Forum

XS
SM
MD
LG