Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 14:38

Blinken kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa NATO mjini Brussels


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.

Afisa wa gazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema Jumatatu kwamba Marekani wiki hii inaungana na mataifa mengine wanachama wa NATO katika kuhimiza dhamira ya Umoja huo ya kuiunga mkono Ukraine kwenye vita vyake dhidi ya uvamizi wa Russia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatatu anaelekea mjini Brussels, ili kuungana na mawaziri wenzake kutoka mataifa ya NATO, ambao wanakutana kuanzia Jumatatu hadi Novemba 29.

Jumatano Blinken ataongoza ujumbe wa Marekani huko Macedonia Kaskazini ambayo ni mwanachama wa NATO, ambako kunafanyikia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka Shirika la Kimataifa la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, OSCE, kwenye mji mkuu wa Skopje.

Marekani itakuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa NATO mjini Washington kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka ujao. Blinken anatarajiwa kuzungumzia vipaumbele vya mkutano huo na wenzake, wakati NATO itakapokuwa ikiadhimisha miaka 75 tangu kubuniwa.

Forum

XS
SM
MD
LG