Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:54

Blinken awasili Afrika Kusini kituo cha kwanza cha ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa ziarani Afrika Kusini.Andrew Harnik /REUTERS.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa ziarani Afrika Kusini.Andrew Harnik /REUTERS.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliwasili Afrika Kusini Jumapili, kituo cha  kwanza cha ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika.

Mbali na Afrika Kusini, Blinken pia ataitembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Blinken anatarajiwa kutoa hotuba muhimu nchini Afrika Kusini Jumatatu kuhusu mkakati wa Marekani kwa afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mabadiliko ya hali ya hewa, biashara, afya na uhaba wa chakula vyote vitakuwa katika majadiliano.

Akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wanasema Blinken atafanya kazi ili kupunguza mivutano kati ya Congo na Rwanda. Congo imemshutumu jirani yake kwa kuliunga mkono kundi la waasi la M23, madai ambayo Kigali inakanusha.

Nchini Rwanda, Blinken atazungumzia "kufungwa kimakosa" kwa mkazi wa kudumu wa Marekani Paul Rusesabagina, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje. Vitendo vya Rusesabagina vilisaidia kuwaokoa mamia ya watu wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na kuhamasisha kutengenezwa filamu ya Hotel Rwanda.

XS
SM
MD
LG