Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 07:13

Blinken ameitembelea Ankara na kuzungumzia uuzaji wa ndege F-16 kwa Uturuki


U.S. Secretary of State Blinken visits Ankara
U.S. Secretary of State Blinken visits Ankara

Bunge la Marekani lazima liidhinishe dola bilioni 20 za uuzaji wa F-16 ambazo zinajumuisha ombi la Uturuki la kununua ndege 40 na takribani vifaa 80 vya kisasa. Blinken alisema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema utawala wa Biden unaunga mkono uuzaji wa ndege za kivita aina ya F-16 kwa Uturuki na alielezea matumaini kwamba wote Sweden na Finland hivi karibuni zitajiunga na muungano wa NATO wakati alipoitembelea Ankara kwa mazungumzo Jumatatu na viongozi wa Uturuki.

Bunge la Marekani lazima liidhinishe dola bilioni 20 za uuzaji wa F-16 ambazo zinajumuisha ombi la Uturuki la kununua ndege 40 na takribani vifaa 80 vya kisasa. Blinken alisema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu kwamba hakuweza kutoa ratiba ya kuliarifu rasmi bunge kuhusu uuzaji uliopendekezwa lakini amekuwa akiwasiliana na utawala wa Biden kuunga mkono suala hilo.

Hii ni muhimu sana kwa ushirikiano unaoendelea wa NATO na katika usalama wa kitaifa wa Marekani, Blinken alisema. Pia anatarajiwa kukutana Jumatatu na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan. Ziara hii imekuja wakati Uturuki na Hungary wanaendelea kuwa wanachama pekee wa NATO ambao hawajaziidhinisha Sweden na Finland kujiunga na umoja huo katika utaratibu ambao lazima uwe wa kauli moja.

XS
SM
MD
LG