Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:20

Biden Kukabiliwa na Changamoto Nzito Katika Utawala Wake


Rais Mteule Joe Biden akizungumza Jumamosi huko Wilimington, Delaware.
Rais Mteule Joe Biden akizungumza Jumamosi huko Wilimington, Delaware.

Mdemocrat Joe Biden atachukua madaraka ya urais wa Marekani wakati ambapo taifa linajitahidi kupambana na janga la Covid 19, uchumi uliotetereka na umma wa Marekani uliogawanyika.

Biden, Makamu Rais wa zamani na Seneta kutoka jimbo la Delaware, aliendesha kampeni yake kwa ahadi ya kutekeleza sera pana ili kupanua fursa kwa huduma za afya na elimu, nyongeza ya mshahara wa kima cha chini na msaada kwa wafanyakazi maskini, na kuendeleza viwanda vya nishati ambavyo vitasaidia kufungua nafasi za mamilioni ya ajira mpya.

Wasi wasi wake mkubwa wa kwanza, hata hivyo, itakuwa kushughulikia ongezeko la janga la virusi vya corona. Jumatatu anatarajiwa kutangaza kikosi kazi chake ambacho kitamshauri rais mteule kuhusu njia za kukabiliana na virusi ambavyo vimeua zaidi ya watu 236,000 nchini Marekani na kuwaambukiza zaidi ya watu milioni 9.8, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

"Tunawexza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi katika miezi kadhaa ijayo," amesema alipohutubia huko Wilmington Ijumaa iliyopita.

Lakini Wachambuzi wanasema changamoto za Biden ni kubwa sana, na mafanikio yake yanategemea kubuni njia za kuiunganisha nchi na kufikia muafaka na warepublican huko Capitol Hill mara Rais Donald Trump atakapoondoka.

"Migawanyiko ni mikubwa sana," amesema David Redlaqsk, profesa wa siasa katika Chuo Kikuu cha Delaware. "Nina matumaini kwamba tutasogea kwenye njia ya kuponya kadri muda unavyokwenda. Hilo halitatokea haraka. Halitatokea kwa urahisi."

Biden alitajwa kuwa mshindi wa urais wa Marekani siku ya Jumamosi, baada ya kupata uongozi mkubwa wa kura katika jimbo la Pennyslvania, ikifuatiwa na ushindi wa huko Nevada. Anatarajiwa kuapishwa Januari 20, 2021.

Baraza la Senate la Republican

Pamoja na kutafuta njia za kukabiliana na janga ambalo limepelekea vifo vya Covid kwa siku kufikia 1,000 kwa muda wa siku chache zilizopita, Biden pia ameweka kipaumbele kutoka kutoa ahueni ya kiuchumi kwa wafanyakazi takriban milioni 20 ambao wamepoteza ajira wakati wa janga la ambalo limedumaza kwa kiasi kikubwa sekta nzima ya viwanda, hasa kuathiri usafiri, majumba ya sinema na migahawa.

Lakini kupitisha ajenda hii, Biden huenda akatakiwa kufikia muafaka na upande wa upinzani, hasa kiongozi wa walio wengi katika baraza la Senate, mrepublican Mitch McConnell wa Kentucky, ambaye ameshinda muhula mwingine wa miaka sita.

"McConnell atakuwa makini kuwemo katika shughuli zinazowataka kufanya maamuzi na kutoruhusu maamuzi mengi ya waliberali, na itamlazimu kufanya mashauriano kwa masuala hayo," amesema Shannon O'Brien, ambaye anafundisha siasa za Marekani katika Chuo Kikuu cha Texas.

Biden ameshinda urais, lakini chama cha Democratic huenda kisiwe na wingi wa kudhibiti baraza la Senate. Wademocrat watahitaji kushinda chaguzi mbili ambazo zinarejewa katika jimbo la Georgia ambalo kiasili ni la warepublican hapo mwezi Januari na kufungana kwa wajumbe 50 kwa 50 katika seneti - na kumuwezesha makamu rais mteule Kamala Harris kupiga kura ya kuvunja kufungana huko na kudai udhibiti wa baraza hilo.

Kama chama cha Biden hakitashinda viti muhimu katika seneti, atakuwa ni rais wa kwanza mpya aliyechaguliwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 100 ambaye chama chake hakina udhibiti katika mabaraza yote mawili ya bunge.

Warepublican wakiwa bado hawana wingi katika Baraza la Wawakilishi, waliongeza viti katika bunge hapo Novemba 3.

Biden, hata hivyo ana historia ndefu kama mbunge aliyekuwa akifikia muafaka wakati wa uhuduma wake wa miongo kadhaa kama seneta na makamu rais wa Barack Obama. Katika nyakati mbali mbali wakati wa utawala wa Obama, Biden alifikia makubaliano ya kupunguza bajeti na McConnell. Ujuzi huo huenda ukamsaidia kukabiliana na mkwamo uliopo Washington.

Biden amesisitiza haja ya kushirikiana pamoja kufanya kazi kwa ajili ya mambo mazuri kwa taifa.

"Tunaweza kuwa wapinzani, lakini siyo maadui," Biden amesema katika hotuba yake.

XS
SM
MD
LG