Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:24

Biden hana nia ya kumfuta kazi waziri wa ulinzi Lloyd Austin; inasema White House


Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin.

Austin ambaye kwa wadhifa yupo chini ya Biden katika  mlolongo wa uongozi wa jeshi la Marekani alilazwa hospitali siku ya mwaka mpya lakini umma haukufahamishwa

Rais wa Marekani Joe Biden hana nia ya kumfuta kazi waziri wa ulinzi, Lloyd Austin baada ya Austin kushindwa kwa siku kadhaa kusema hadharani kuwa amelazwa hospitali na bado hajafichua suala lake la kiafya, White House imesema Jumatatu.

“Hakuna mpango kwa kitu kingine chochote isipokuwa kwa Waziri Austin kuendelea na kazi”, msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa, John Kirby aliwaambia waandishi wa habari.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin

Austin, ambaye kwa wadhifa yupo chini ya Biden katika mlolongo wa uongozi wa jeshi la Marekani, alilazwa hospitali siku ya mwaka mpya, lakini matatizo yalijitokeza katika kile kilichoelezwa kama utaratibu wa matibabu wa kuchagua, ambao aliupanga hapo Desemba 22.

Msemaji wa Pentagon, Meja Jenerali Patrick Ryder alisema kuwa “hakuna wakati wowote usalama wa taifa ulikuwa hatarini” kwa sababu ya Austin kulazwa hospitali, ingawa majukumu yake yalihamishiwa kwa Naibu Waziri wa Ulinzi Kathleen Hicks wakati Austin alipolazwa hospitali. Msemaji wa serikali amesema Austin “hana mpango wa kujiuzulu”.

Forum

XS
SM
MD
LG