Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 00:56

Bensouda:Hakuna kinga ya ICC kwa Kenyatta na Ruto


Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC
Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, Fatou Bensouda, Jumatatu ameonya kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na mbunge wa Eldoret kaskazini William Ruto hawatapatiwa kinga hata kama wanashinda katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwakani.

Bi Bensouda alisema kwamba taratibu za kisiasa nchini Kenya hazitavuruga taratibu za sheria za ICC ambapo alisisitiza kwamba taratibu hizo zitaendelea bila kuingiliwa.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari mjini Nairobi, Bensouda alisema mahakama haina mpango wa kupanga tena kalenda yake ili kutoa njia kwa ajili ya uchaguzi wa Kenya ambapo Kenyatta na Ruto ni washiriki wakuu.

“Hakuna kinga kwa uhalifu wa kimataifa kwenye ICC. Kalenda ya sheria kwenye mahakama haitabadilishwa. Majaji wa ICC hawayumbishwi na taratibu zozote za kisiasa,” alisema Bensouda.

Bwana Kenyatta na bwana Ruto ni wahusika muhimu katika uchaguzi mkuu ujao. Wanasiasa hao wawili pia wameanzisha ushirikiano kwenye uchaguzi mkuu ili kuongeza nafasi zao za kushinda.

Mwendesha mashtaka huyo anatarajiwa kukutana na maafisa wa serikali nchini Kenya akiwemo Rais Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga, wabunge katika kamati ndogo iliyochaguliwa na ICC, Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu.
XS
SM
MD
LG