Akizungumza mjjini Washington DC mbele ya kamati ya baraza la wawakilishi kuhusu masuala ya sheria mjini Washington, Barr alisema maandamano yanayoendelea kwa sasa hayana uhusiano wowote na kifo cha Mmarekani mweusi, George Floyd, kilichotokea kwenye mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota, mnamo mwezi Mei mwaka huu.
Wakati wa kikao hicho ambacho kiligubikwa majibizano yenye cheche za maneno, wabunge wa mrengo wa chama cha Demokratic walimshutumu Barr, kwamba anaminya haki za Wamarekani za kfanya maandamano na kwamba anachukua hatua ambazo zinaunga mkono kampeni ya kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump mwezi Novemaba mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Jerrold Nadler, alimshutumu Barr kwa kile alichokiita "kuwatia hofu Wamarekani kote nchini" kwa kupeleka maafisa hao kwa miji ambako, viongozi wao hawakutaka wapelekwe.
“Ni aibu kubwa kwako,” alisema Nadler.
Barr ndiye Mwanasheria Mkuu wa pili kuhudumu katika utawala wa Trump baada ya mwanasheria mkuu wa kwanza Jeff Sessions, kuulizwa na rais huyo ajiuzulu.
Barr amekuwa akikabiliwa na shutuma mbalimbali, hususan kutoka kwa Wademokrat, kwamba anatekeleza majukumu yake kulingana na vile Rais Trump anataka, na wala siyo kwa mujibu wa sheria na kwa manufaa ya Wamarekani wote kama inavyostahili.