Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:10

Ayatollah Khamenei anatoa wito mataifa ya kiislam kukata uhusiano na Israel


Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi mkuu wa kidini wa Iran. Nov. 19, 2023. (Office of Iran's Supreme Leader/West Asia News Agency via Reuters)
Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi mkuu wa kidini wa Iran. Nov. 19, 2023. (Office of Iran's Supreme Leader/West Asia News Agency via Reuters)

Baadhi ya serikali za Kiislamu zimelaani uhalifu wa Israel katika mikutano mbali mbali wakati baadhi yao hawajafanya hivyo. Hili halikubaliki, alisema Khamenei kabla ya kusisitiza kuwa jukumu kuu la serikali za Kiislamu ni kusitisha nishati na bidhaa nyingine kwenda Israel

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei ametoa wito kwa mataifa ya Kiislamu yenye uhusiano wa kisiasa na Israel kukata mahusiano kwa kipindi fulani, vyombo vya habari vya kitaifa vimeripoti Jumapili, ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kutoa wito wa vikwazo vya mafuta na chakula dhidi ya Israel.

Baadhi ya serikali za Kiislamu zimelaani uhalifu wa Israel katika mikutano mbali mbali wakati baadhi yao hawajafanya hivyo. Hili halikubaliki, alisema Khamenei kabla ya kusisitiza kuwa jukumu kuu la serikali za Kiislamu ni kusitisha nishati na bidhaa nyingine kwenda Israel. Serikali za Kiislamu zinapaswa angalau kusitisha uhusiano wa kisiasa na Israel kwa muda kadhaa, alisema Khamenei.

Wakati wa mkutano wa pamoja kati ya wanachama wa Umoja wa nchi za Kiislamu na Umoja wa Nchi za Kiarabu katika mji mkuu wa Saudi Arabia hapo Novemba 11, mataifa ya Kiislamu hayajakubali kuiwekea Israel vikwazo vingi, kama ilivyoombwa na Rais wa Iran Ebrahim Raisi.

Forum

XS
SM
MD
LG