Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 05:08

AU inashindwa kuchukua hatua kuzuia ghasia Misri


Wafuasi wa rais wa Misri aliyepinduliwa Mohamed Morsi wakibeba mabango yanayoonesha waathiriwa wa uvamizi wa kijeshi dhidi ya makambi yao Cairo. August 23, 2013.
Wafuasi wa rais wa Misri aliyepinduliwa Mohamed Morsi wakibeba mabango yanayoonesha waathiriwa wa uvamizi wa kijeshi dhidi ya makambi yao Cairo. August 23, 2013.
Wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood la Misri hapo Ijumaa waliingia kwenye mitaa ya Cairo wakitowa wito wa kuondolewa serikali ya muda inayoungwa mkono na jeshi na kumrudisha madarakani rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi.

Maandamano hayo yalikuwa ya kwanza kufanywa na wanachama wa Brotherhood katika muda wa siku kadhaa na hayakuonekana kuwa na hamasa wala idadi kubwa ya watu kama maandamano ya awali.
please wait

No media source currently available

0:00 0:22:03 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Live Talk Idhaa ya Kiswahili ilizungumzia hali hiyo ya kisiasa hasa kufuatia kutolewa gerezani rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani kitendo ambacho kimesababisha kundi la Muslim Brotherhood kuitisha maandamano makubwa nchini humo kupinga jambo hilo ambalo limesababisha hisia mbali mbali kujitokeza huko.

Matukio haya ya Misri pia yamezusha wasiwasi mkubwa katika nchi za kiafrika, nchi za kiislam na za ulaya. Mwalimu Bashiru Ally, wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, anasema hadhani Umoja wa afrika utaweza kuchukua hatua yeyote kusaidia kutanzua mzozo wa Misri, ukichukulia yaliyotokea Libya na Tunisia.

Anasema, “kusema kweli kutakuwa hakuna hatua za dhati na madhubuti kwa hali ilivyo sasa, hakuna, kwa sababu kama kungelikuwepo wangeshaingia na tungeshaona aina Fulani ya kuingilia kati ili kuzuai mauwaji.”
XS
SM
MD
LG