Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 03:46

Argentina yabeba kombe la dunia


Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi akinyanyua kombe la dunia pamoja na wachezaji wenzake wakisherehekea kushinda Kombe la Dunia. Lusail Stadium, Lusail, Qatar - December 18, 2022 . Reuters.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi akinyanyua kombe la dunia pamoja na wachezaji wenzake wakisherehekea kushinda Kombe la Dunia. Lusail Stadium, Lusail, Qatar - December 18, 2022 . Reuters.

Timu ya Argentina imefanikiwa kutwaa taji la dunia baada ya kuishinda Ufaransa kwa penati 4-2 katika uwanja wa Lusille Doha Qatar Jumapili.

Penalti hizo zilifuata baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 2-2 katika muda wa dakika 90 ambapo ilionekana kana kwamba Argentina wameshinda mchezo huo baada ya kuongoza kwa bao 2-0 hadi dakika ya 80.

Mabao ya Argentina yalifungwa na Lionell Messi kwa penalti katika dakika ya 23 na mchezaji mkongwe Angel Fabian Di Maria akaongeza bao la pili katika dakika ya 36.

Lakini wakati washabiki wakifikiri Argentina wamemaliza mchezo walishangazwa kama ambavyo ilitokea katika mechi ya Uholanzi lakini safari hii magoli haya mawili yalirudishwa haraka sana katika kipindi cha dakika mbili, kwani katika ya 80 Ufaransa walipata penalti na Kylian Mbape akaweka mpira kimiani.

Haikushia hapo kwani alikuwa ni Mbappe tena katika dakika ya 81 mchezaji huyu mahiri wa PSG alipachika bao la pili kwa mkwaju mkali uliomshinda golikipa machachari wa Argentina Damian Emiliano Martinez na kupelekea mpira Kwenda dakika 30 za nyongeza.

Dakika hizo tena zilikuwa za moto kwani alikuwa ni Lionell Messi tena aliyepachika bao la 3 kwa Argentina katika dakika ya 107 lakini Ufaransa walindelea kupambana na kushuhudia wakigoma kutolewa kirahisi na katika dakika ya 118 Mbappe aliwainua washabiki wa Ufaransa akiwamo rais wao Emmanuel Macron kwa kupachika penati nyavuni na kusawazisha ikawa 3-3 na hivyo mchezo ukandelea kwenye penlti tano tano.

Katika penati kipa wa Argentina alikuwa shujaa baada ya kutoa penalti mbili na hivyo kupelekea timu yake kupata ushindi wa jumla ya mabao 4-2.

Ushindi huo uliihakikishia Argentina taji la tatu la Kombe la Dunia katika historia yao na la kwanza tangu 1986. Hilo ni taji la kwanza la Lionel Messi la Kombe la Dunia huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 akipongezwa na wachezaji wenzake kwenye kipenga cha mwisho huku kukiwa na machozi, utulivu na furaha isiyozuilika.

Historia yajirudia kombe la dunia laamuliwa kwa penalti

Historia imeandikwa hivi ndivyo ilivyo. Na mchezo huu ulifikisha moja ya fainali kubwa za kimchezo kuwahi kutokea kwani kwa mara ya tatu tu katika historia, Kombe la Dunia liliamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Wakati ulipofika wa kubeba kombe fataki zililipuka na takriban watu 80,000 wakiunguruma na kuimba Lionel Messi alitabasamu. Jezi yake ya Argentina iliyofunikwa na joho jeusi la Emir wa Qatar aliyempatia kwa heshima ikiwa ni alama iliyotengwa kwa ajili ya maafisa wakuu na masheikh. Messi alitabasamu kisha akainua juu Kombe la Dunia, ndoto ya maisha yake ilitimia.

Wachambuzi wanasema ule mjadala wa Messi na Ronaldo sasa umekwisha na Mesi amethibitisha ndiye mchezaji bora wa wakati wote.

XS
SM
MD
LG