Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:01

Afrika Kusini yafanya uchunguzi wa fedha kutoka Nigeria.


Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma akiwa na mkewe. katika picha .
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma akiwa na mkewe. katika picha .

Serikali ya Afrika kusini inachunguza kugunduliwa kwa dola million 9.3 fedha taslim ambazo maafisa wa forodha walizipata kwenye mzigo kutoka kwenye ndege binafsi iliyoingia kutoka Nigeria.

Ugunduzi huo ulifanyika September 5 kwenye uwanja wa ndege wa Lanseria, kaskazini magharibi mwa Johannesburg, baada hitilafu kugunduliwa kwenye mizigo ya raia wawili kutoka Nigeria na Mwingine kutoka Israel ambao walikuwa kwenye ndege.

Maafisa wa forodha walisema walizitaifisha fedha hizo zilizokuwa zimefungwa kwenye mabunda 90 ya takriban dola laki moja kila moja, katika masanduku mawili meusi.

Idadi ya fedha anazoruhusiwa abiria Afrika kusini ni takriban dola elfu 2 mia 3. Bado hakuna aliyekamatwa.

Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa fedha hizo zilikuwa za ununuzi wa silaha kwa idara ya ujasusi ya Nigeria, na kwamba mmoja wa wanaume kwenye ndege hiyo alikuwa na waraka wa bidhaa zilizotakiwa kununuliwa huko Afrika kusini.

Kwa sasa, fedha hizo zimekabidhiwa benki ya akiba kuhifadhiwa hadi uchunguzi utakapokamilika.

XS
SM
MD
LG