Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:47

Afrika haina mfumo thabiti wa kuandikisha wanaozaliwa na wanaofariki


Mawaziri wa masuala ya jamii kutoka nchi mbali mbali za Afrika wakutana mjini Addis Abeba kujadili kwa mara ya kwanza tatizo kubwa la kukosekana mfumo thabiti wa kuandikisha wanaozaliwa na wanaofariki.

Mkutano huo wa siku mbili unajadili kile kinachosemekana kua ni "kashfa ya kutojulikana raia", tatizo linalotokana na ukosefu wa habari za uhakika juu ya vifo vinavyotokea nchini au watoto wanaozaliwa.

Nchi nyingi za kiafrika hazina mfumo thabiti wa kuandikisha wanaozaliwa na wanaofariki. Watalaam wanasema idadi tunazosikia kuhusu wanawake wanofariki wakati wa kujifungua, au vifo kutokana na ukimwi na malaria, au watoto wanajeshi na wasichana wanoolewa wadogo, mara nyingi idadi hizo ni za kukadiriwa tu.

Dmitri Sanga, kaimu mkurugenzi wa kituo cha takwimu cha Afrika, huko Addiss Ababa, anasema serikali nyingi za Afrika zina habari chache kabisa zilizo sahihi kuhusu wananchi wao.

"Sio tu tatizo kwa mtu binafsi,lakini pia kwa familia yake,kwa serikali na kadhalika, kwa hivyo ikiwa wanataka kupanga kuboresha maisha ya watu, lazima wajuwe idadi ya watu wlioko. Lazima wajuwe watu wangapi wanafariki na kutokana na ugonjwa gani. Kwa hivyo rekodi sahihi za watoto wanozaliwa, vifo na shughuli nyenginezo muhimu, ndio chanzo cha kuimarisha mfumo huo."

Ukosefu wa kuwepo kwa rekodi sahihi kunatatiza kazi za wasomi na waandishi habari wanojaribu kufahamu kiwango cha matatizo ya Afrika, na kiwango cha kasi ya maendeleo yake.

XS
SM
MD
LG