Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 20, 2025 Local time: 23:51

Mechi za robo fainali zakamilika, mmh moja mezani


Wachezaji wa Cameroon wakishangilia goli lao dhidi ya Senegal Jan 28
Wachezaji wa Cameroon wakishangilia goli lao dhidi ya Senegal Jan 28

Hatimaye, baada ya karibu wiki mbili za michuano ya awali robo fainali za kombe la mataifa ya Afrika zimekamilika ingawa moja itapangwa mezani baada ya Mali na Guinea kumaliza mechi zao za kundi D zikiwa zimefungana kwa kila namna.

Mechi za mwisho Jumatano ziliiona Ivory Coast ikijikatia tiketi ya robo fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cameroon huko Malabo katika mechi pekee ya kundi hilo ambayo haikumalizika kwa sare ya 1-1. Kundi D hasa ndio lilikuwa kundi la kifo kwani mechi tano kati ya sita ziliishia na sare a 1-1.

Timu hizo - Ivory Coast, Senegal, Mali na Guinea - ziliingia katika mechi zao za mwisho leo zote zikiwa na pointi 2 kila moja na idadi sawa ya magoli. Ushindi wa Ivory Coast uliiwezesha kungoza kundi hilo kwa pointi 5 wakati sare ya 1-1 ya iliwaacha Mali na Guinea zikiwa zimefungana tena kwa pointi tatu kila moja.

Max Alain Gradel wa Ivory Coast akishangalia goli lake dhidi ya Senegal
Max Alain Gradel wa Ivory Coast akishangalia goli lake dhidi ya Senegal

Sasa mshindi wa pili katika kundi hilo atachaguliwa mezani kwa bahati nasibu itakyaochezeshwa Alhamisi kuamua nani atakutana na Ghana katika robo fainali moja Februari mosi mjini Malabo.

Mechi nyingize za robo fainali itakuwa kati ya mahasimu wa jadi DRC na Congo Brazzaville siku ya Jumamosi – miji ya Kinshasa na Brazzaville ambayo inatenganishwa na mto Congo kwa umbali wa chini ya maili moja itawaka moto siku hiyo. Jumamosi hiyo hiyo wenyeji Equatorial Guinea wanapambana na Tunisia katika robo fainali ya pili, mechi zote zitachezwa mjini Bata.

Ivory Coast itachuana na Algeria katika robo fainali ya pili ya mjini Malabo Jumapili. Nusu fainali zimepangwa kucheza Jumatano ijayo, Februari 4, wakati fainali itapigwa Februari 8 mjini Bata.

XS
SM
MD
LG