Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:10

Chris Christie asitisha kampeni zake za kuwania urais Marekani 2024


Chris Christie, gavana wa zamani wa jimbo la New Jersey kwa chama cha Republican
Chris Christie, gavana wa zamani wa jimbo la New Jersey kwa chama cha Republican

“Ni wazi kwamba hakuna njia ya mimi kushinda uteuzi, ndio maana nasitisha kampeni yangu kuwania nafasi ya rais wa Marekani".

Gavana wa zamani wa jimbo la New Jersey nchini Marekani, Chris Christie amesema Jumatano kwamba anasitisha azma yake ya kugombea urais kupitia chama cha Republican, siku chache kabla ya uchaguzi wa Iowa katika juhudi za mwisho za kumnyima Donald Trump kupata uteuzi.

“Lengo langu halijawahi kuwa sauti tu dhidi ya chuki na mgawanyiko pamoja na ubinafsi wa kile ambacho chama chetu kimekuwa, chini ya Donald Trump,” Christie alisema katika mkutano huko New Hampshire. “Siku zote nimekuwa nikisema kwamba kama ungetokea wakati katika kinyang’anyiro hiki ingetokea sikuweza kuona njia ya kufanikisha lengo hilo, hivyo ningejitoa,” alisema.

“Ni wazi kwangu hivi leo usiku kwamba hakuna njia ya mimi kushinda uteuzi, ndio maana nasitisha kampeni yangu usiku wa leo kuwania nafasi ya rais wa Marekani.”

Haikubainika wazi iwapo Christie atamuunga mkono mmoja wa wapinzani wake, lakini alisikika akimkosoa balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley, katika mazungumzo ya moja kwa moja yalioandaliwa na kampeni yake kabla ya tukio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG