Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:38

Mji wa St Louis Park wapata meya mwenye asili ya Kisomali


Nadia Mohamed (Kwa hisani ya Facebook)
Nadia Mohamed (Kwa hisani ya Facebook)

Mji wa St Louis Park umekuwa wa pili Jumanne nchini Marekani kumchagua Meya Mmarekani mwenye asili ya Kisomali.

Nadia Mohammed akizungumza na Wamarekani wenye asili ya Kisomali baada ya kushinda uchaguzi wa meya wa kihistoria, Minnesota Jumanne, Novemba 7, 2023
Nadia Mohammed akizungumza na Wamarekani wenye asili ya Kisomali baada ya kushinda uchaguzi wa meya wa kihistoria, Minnesota Jumanne, Novemba 7, 2023

Mjumbe wa baraza la mji huo Nadia Mohamed mwenye umri wa miaka 27 ameshinda kwa kura nyingi dhidi ya Dale A.

Nadia mfanyakazi wa zamani wa benki katika uchaguzi Jumanne amekuwa meya wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Kisomali na vile vile mtu mweusi katika mji wa St. Louis Park, Minneapolis.

Mohamed alizungukwa na dazani ya wafuasi wake katika kituo cha Westwood Hills Nature, wakati tangazo lilipotolewa.

Nadia Mohamed alisema: “ Hii ina maana kubwa sana kwangu, inamaanisha kwamba tunapata uwakilishi ambao tunastahili, najisikia vizuri kuwa meya wa mji ambao nilihamia miaka 18 iliyopita na kuwa meya wa kwanza mweusi, kuwa meya wa kwanza msomali na meya kijana.”

Forum

XS
SM
MD
LG