Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:28

Wademocrat wamepata ushindi mzuri uchaguzi wa Marekani katikati ya muhula


Wapiga kura wakitumia haki yao katika uchaguzi mdogo huko Columbus kwenye jimbo la Ohio. November 7, 2023.
Wapiga kura wakitumia haki yao katika uchaguzi mdogo huko Columbus kwenye jimbo la Ohio. November 7, 2023.

Wapiga kura katika jimbo la Ohio waliidhinisha marekebisho ya katiba yanayohakikisha upatikanaji wa fursa za utoaji mimba na aina nyingine za huduma za afya ya uzazi.

Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ujao wa rais, Wademocrat na watetezi wa haki za utoaji mimba walishinda katika uchaguzi kwenye majimbo kadhaa ya Marekani jana Jumanne.

Wapiga kura katika jimbo la Ohio waliidhinisha marekebisho ya katiba yanayohakikisha upatikanaji wa fursa za utoaji mimba na aina nyingine za huduma za afya ya uzazi. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani mwaka jana wa kubadilisha uamuzi wa Roe v. Wade wa mwaka 1972 ambao ulikuwa umelinda haki za utoaji mimba.

Ohio ilikuwa moja ya majimbo kadhaa ambako marufuku ya utoaji mimba ilianza kutekelezwa ikiwa ni matokeo ya uamuzi wa mahakama. Kabla ya Ohio, wapiga kura katika majimbo mengine, pamoja na California, Kansas, Kentucky, Michigan, Montana na Vermont, walipitisha juhudi za kulinda fursa ya utoaji mimba kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu mwaka jana wa 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG