Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:03

Rais wa Ukraine yupo Finland kuhudhuria mkutano wa Nordic


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy

Ziara ya Zelenskyy nchini Finland inakuja wiki chache baada ya taifa hilo la Nordic kukubaliwa kama taifa la 31 kuwa wanachama wa NATO

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amewasili nchini Finland leo Jumatano kushiriki mkutano wa kilele na viongozi wa mataifa matano ya Nordic.

Zelenskyy atakutana na Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson, Jonas Gahr Støre wa Norway, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen na Katrín Jakobsdóttir wa Iceland, katika makazi rasmi ya Rais wa Finland Sauli Niinistö. Ziara ya Zelenskyy nchini Finland inakuja wiki chache baada ya taifa hilo la Nordic kukubaliwa kama taifa la 31 kuwa wanachama wa NATO.

Helsinki ilitafuta uanachama katika muungano huo wa kijeshi wenye makao yake Magharibi kujibu uvamizi wa Moscow nchini Ukraine uliofanyika Februari mwaka jana.Wakati huo huo, kituo cha mafuta kusini mwa Russia kilishika moto mapema Jumatano asubuhi. V

eniamin Kondratyev, gavana wa mkoa wa kusini magharibi mwa Russia wa Krasnodar, aliandika kwenye APP ya Telegram kwamba kituo hicho kilikuwa katika kijiji cha Volna. Gavana Kondratyev alisema hakuna ripoti za vifo kutokana na moto huo.

XS
SM
MD
LG