Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:09

Mfalme Charles wa Uingereza hatohudhuria mkutano wa Misri


Mfalme Charles III wa Uingereza. Sept. 10, 2022.
Mfalme Charles III wa Uingereza. Sept. 10, 2022.

Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza hatohudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia wa mabadiliko ya hali ya hewa nchini Misri mwezi ujao, chanzo cha kifalme kimesema Jumapili, wakati mfalme huyo mpya akijiondoa katika majukumu yake ya awali ya kampeni.

Kasri ya Buckingham ilitafuta ushauri wa serikali kuhusu mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa COP27 na ilikubaliwa kwa kauli moja kwamba haitakuwa sahihi kwa Charles kwenda huko kwa kile ambacho itakuwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi, kilisema chanzo hicho.

Hakuna uthibitisho kwamba Charles huenda angehudhuria mkutano huo kabla ya kuwa mfalme mwezi uliopita kufuatia kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth, kilisema chanzo hicho.

Charles alizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kilele wa COP26 huko Glasgow mwaka 2021, ambao aliuelezea kama "hatua ya mwisho" ya kuuokoa ulimwengu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, baada ya malkia kujiondoa kwa ushauri wa madaktari.

XS
SM
MD
LG