Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 20:26

Mapigano ya risasi kati ya magenge hasimu huko Haiti yamesababisha vifo vya watu 50


Mwanachama katika ushirika wa genge la G9 akitoa silaha zilizohifadhiwa kwenye mji mkuu Port-au-Prince, Haiti, Oct. 6, 2021.
Mwanachama katika ushirika wa genge la G9 akitoa silaha zilizohifadhiwa kwenye mji mkuu Port-au-Prince, Haiti, Oct. 6, 2021.

Mapigano ya risasi kati ya magenge hasimu yamesababisha vifo vya watu 50 tangu Ijumaa karibu na mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince, Meya wa eneo hilo alisema Jumatatu huku ghasia zikiendelea kusambaa katika taifa hilo la Caribbean.

Mapigano ya risasi kati ya magenge kwenye kitongoji maskini cha Cite Soleil, pia yamesababisha zaidi ya watu 100 kujeruhiwa, kulingana na Meya wa Cite Soleil, Joel Janeus, akiongeza kwamba 50 kati ya hao wako katika hali mbaya.

Magenge hayo pia yamezuia ufikiaji wa kituo cha mafuta cha Varreux gazeti la Haiti Le Nouvelliste liliripoti. West Indies Group, kundi la Haiti ambalo linamiliki uwanja wa Varreux halikujibu mara moja ombi la kutoa maoni yao.

Ofisi ya waziri mkuu, Ariel Henry, haikujibu mara moja ombi la maoni hayo. Ghasia hizo zinaonekana kuwa matokeo ya makabiliano kati ya G9 na magenge ya GPEP.

Ghasia za magenge zimeongezeka tangu Rais Jovenel Moise, alipouawa mwaka mmoja uliopita katika uvamizi uliofanyika usiku, na kusababisha vuguvugu la kisiasa na makundi ya uhalifu kupanua udhibiti wao katika eneo la nchi hiyo.

Wanaharakati wa haki mwezi Mei walisema mapigano kati ya mpinzani Chen Mechan na magenge 400 ya Mawozo yamesababisha vifo vya watu 148, baadhi yao walikufa kwa kukatwakatwa kwa mapanga au walifariki wakati nyumba zao zilipochomwa moto.

XS
SM
MD
LG