Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:42

Uvamizi wa Russia nchini Ukraine huwenda ukachukua muda mrefu; inasema idara za kijasusi Marekani


Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye vifaru katika barabara ya Donbas mashariki mwa Ukraine. June 21, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye vifaru katika barabara ya Donbas mashariki mwa Ukraine. June 21, 2022.

Idara za kijasusi za Marekani zimefikia uwamuzi kwamba uvamizi wa Russia nchini Ukraine huenda ukaendelea kwa muda mrefu lakini kwamba wanajeshi wa Moscow huwenda katika muda mfupi hawataweza kusonga mbele zaidi ya jimbo la mashariki mwa Ukraine.

Mkurugenzi wa idara ya kitaifa ya ujasusi Avril Haines aliuambia mkutano kuhusu mfumo wa usafirishaji bidhaa nje kwamba Russia inadhibiti takribani asilimia 20 ya mali ya Ukraine kwenye mstari wa migogoro unaotanda hadi kilomita 1,100.

Lakini Haines alisema kuwa upinzani wa waasi wa Ukraine katika mikoa inayokaliwa na Russia unaongezeka na hivyo kufanya iwe vigumu kwa Russia kusonga mbele zaidi ya wilaya ya Donbas upande wa mashariki ambako imeteka karibu mkoa mzima wa Luhansk lakini kidogo zaidi kuliko mkoa jirani wa Donetsk.

Suluhu ya amani pia haiwezekani, alisema. Uwezekano mkubwa Haines alisema ni kwamba mzozo huo ambao sasa uko katika mwezi wake wa tano unaendelea kuwa mapambano makali ambayo wa-Russia wanapata mafanikio ya hatua kwa hatua lakini haipati ushindi kamili.

XS
SM
MD
LG