Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:17

Mwakilishi wa UN kwa Congo anasema waasi wa M23 wana silaha na vifaa vya kijeshi vya kutosha


Bintou Keita mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC
Bintou Keita mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Bintou Keita alisema Jumatano kwamba waasi walioibuka tena wa kundi la M23 huko mashariki mwa nchi hiyo wana silaha na vifaa vya kijeshi vya kutosha na hivyo wanasababisha tishio kwa raia.

Keita Mkuu wa MONUSCO huko Congo amesema wakati wa mapigano ya hivi karibuni M23 imekua ikiendesha shughuli zake kama jeshi la kawaida kuliko kundi lenye silaha. Aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kundi hilo linazidi kupata silaha za kisasa, hasa mizinga ya kushambulia mbali pamoja na vifaa vinavyoweza kufyatua ndege.

Kundi la M23 lilishindwa na jeshi la Congo (FARDC) na wanajeshi maalum vya MONUSCO mwaka 2013. Lakini Novemba mwaka 2021 wapiganaji wake walianza kuibuka tena.

Maafisa wa Congo wanailaumu nchi jirani ya Rwanda wakisema inaliunga mkono kundi hilo ambalo linadaiwa kuwalinda watutsi walio wachache mashariki mwa DRC.

Serikali ya Rwanda inaongozwa na watutsi lakini inakanusha uhusiano wowote na kundi la waasi hao.

XS
SM
MD
LG