Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:18

Wahamiaji 14 wamefariki baada ya boti waliokuwa wakisafiria kushika moto Senegal


Mfano wa boti iliyobeba wahamiaji pamoja na wageni ambayo ilipata ajali nchini Senegal
Mfano wa boti iliyobeba wahamiaji pamoja na wageni ambayo ilipata ajali nchini Senegal

Takribani wahamiaji 14 wamefariki wakati boti waliokua wanasafiria iliposhika moto katika jimbo la kusini la Senegal la Kasamance.

Meya wa mji wa pwani wa Kafountine katika jimbo la Kasamance David Diatta ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne kwamba walifanikiwa kupata mili ya watu hao 14 baada ya tukio hilo la moto siku ya Jumatatu. Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka aliongeza.

Muuguzi mkuu wa mji huo Bourama Faboure alisema kwamba watu 21 wamejeruhiwa wakiwemo wane waliopata majeraha ya moto. Boti hiyo ilikuwa imebeba kiasi cha watu 140 na takribani watu 90 kati yao walionusurika walitambuliwa.

Diatta alisema watu hao walikuwa raia kutoka nchini Guinea, Nigeria, Gambia na Senegal.

XS
SM
MD
LG