Mtawala mkuu wa Saudi Arabia mwana mfalme Mohammed bin Salman alikutana rasmi na viongozi wa Misri, Jordan na Uturuki wiki hii. Lengo lake wanasema wachambuzi ni kuunganisha nafasi zao katika masuala ya usalama kama vile wasiwasi unaoongezeka juu ya Iran. Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na Saudi Arabia mzalishaji mkuu wa mafuta. Ilikuwa sehemu ya ziara hiyo wachambuzi wanasema huku janga la COVID-19 na uvamizi wa Russia nchini Ukraine unaendelea kuwa na athari kubwa.
Ziara ya mwana mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman wiki hii katika eneo hilo, wachambuzi wanasema inaashiria azma yake ya kutambuliwa katika jukwaa la ulimwengu na kumaliza miaka kadhaa ya kutengwa kimataifa kufuatia mauaji ya mwaka 2018 na kukatwakatwa kwa mkosoaji wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi mjini Istanbul ambapo mkuu huyo amekanusha kuhusika binafsi.
Rais wa Marekani Joe Biden aliitaja Saudi Arabia kama isiyo na ushawishi wakati alipofanya kampeni lakini nchi hizo mbili ni washirika wa kihistoria.
Mchambuzi raia wa Jordan, Al Sabaileh ameiambia VOA kwamba vita vya Russia nchini Ukraine, vimesukuma kupanda kwa bei ya mafuta na kusababisha uhaba wa chakula duniani, vimefungua kwa Saudi Arabia mabadiliko katika sheria za ushirikiano na utawala wa Marekani. Saudi Arabia ndio muuzaji mkubwa wa mafuta duniani.
Mchambuzi katika kituo cha Stimson chenye makao yake Washington, Al Sabaileh anasema kwamba ushiriki wa Rais Biden katika mkutano wa Julai 16 huko Jeddah unaowakutanisha pamoja viongozi wa nchi sita za baraza la ushirikiano wa Ghuba (GCC) pamoja na wale kutoka Jordan, Misri na Iraq unampa Bin Salman kama anavyojulikana MBS hadhi fulani na uwezo wa kusaidia kuweka ajenda ya kikanda hasa kwa Iran na Israel. Saudi Arabia ni mmoja wa wanachama wa GCC.
Marekani iliafiki makubaliano ya Abraham mwaka 2020 na kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Israel na mataifa ya Ghuba ya Umoja wa falme za kiarabu na Bahrain. Hakuna nchi iliyowahi kuwa na vita na Israel, tofauti na Misri na Joedan ambazo zilitia saini mikataba ya Amani na taifa la kiyahudi mwaka 1979 na 1994.