Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:07

DRC inaishutumu Rwanda kuwasaidia waasi wa M23 katika mashambulizi ya Bunagana


Wapiganaji wa kundi la M23 wakiwa mashariki mwa DRC katika picha iliyochukuliwa miaka ya nyuma
Wapiganaji wa kundi la M23 wakiwa mashariki mwa DRC katika picha iliyochukuliwa miaka ya nyuma

Mamlaka katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ilisema wanajeshi wa Rwanda wakiwa na silaha walisaidia mashambulizi yanayofanywa na kundi la waasi wa M23 siku ya Jumapili huku DRC ikiwashutumu Rwanda kwa kutaka kuuteka mji wa mpakani wa Bunagana.

Ghasia hizo ziliwasukuma zaidi ya watu 25,000 kukimbia eneo hilo huku maelfu wakitorokea nchi jirani ya Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu (OCHA) lilisema.

Shutuma zinazotolewa na Congo ni sehemu ya mzozo unaoongezeka kati ya majirani hao ambao wamefufua chuki za zamani. Rwanda inakanusha kuunga mkono mashambulizi yanayofanywa na M23.

Ofisi ya gavana wa jimbo la Kivu kaskazini ilisema kuwa vikosi vya Congo vimezuia mashambulizi ya mapema asubuhi Jumapili yaliyofanywa na M23 yakisaidiwa na vikosi vya Rwanda karibu na mji wa Bunagana na kwingineko.

XS
SM
MD
LG