Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:27

Maseneta Marekani wametangaza muundo wa pande mbili unaohusu umiliki wa bunduki


Maandamano yanayodai mageuzi katika sheria ya umiliki wa bunduki yamefanyika kwenye mji wa Washington, DC na kwingineko nchini Marekani
Maandamano yanayodai mageuzi katika sheria ya umiliki wa bunduki yamefanyika kwenye mji wa Washington, DC na kwingineko nchini Marekani

Maseneta wametangaza muundo wa pande mbili siku ya Jumapili katika kujibu mashambulizi ya bunduki kwa umma ya mwezi uliopita ikiwa mafanikio ya kawaida yanayotoa hatua za udhibiti wa bunduki na kuongeza juhudi za kuboresha usalama katika shule na program za afya ya akili.

Pendekezo hilo lipo kwenye hatua kali zilizoangaziwa kwa muda mrefu na Rais wa Marekani Joe Biden na wa-Democrat wengi. Hata hivyo kama makubaliano haya yatapelekea kupitishwa kuwa sheria inaweza kuashiria mabadiliko kutoka mauaji ya bunduki ya miaka kadhaa ambayo yameleta mwamko kidogo kutokana na kukwama katika bunge.

Viongozi wanatarajia kusukuma haraka makubaliano yoyote kuwa sheria wakiwa na matumaini itakuwa mwezi huu kabla ya kasi ya kisiasa kufifia ambayo imechochewa na ufyatuaji risasi wa umma wa hivi karibuni katika mji wa Buffalo katika jimbo la New York na jingine mji wa Uvalde katika jimbo la Texas.

Katika hatua iliyoonekana kama maendeleo makubwa maseneta 20 wakiwemo 10 kutoka chama cha Republican walitoa taarifa ya kupitishwa. Huenda hiyo ni ishara muhimu kwa sababu kikwazo kikubwa zaidi cha kupitishwa kwa hatua hiyo pengine ni katika baraza la seneti ambapo kila upande una viti 50 kwa 50 na hivyo zinahitajika kura 10 za wa-Republican kufikia kiwango cha kawaida cha kura 60 ili mswaada uweze kuidhinishwa.

XS
SM
MD
LG