Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:26

Afisa wa Umoja wa Mataifa asikitishwa na hatua ya serikali ya kijeshi ya Mali


Askari wa Malia wakifanya doria karibu na mpaka wa Niger huko Dansongo Circle
Askari wa Malia wakifanya doria karibu na mpaka wa Niger huko Dansongo Circle

Afisa wa ngazi ya juu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika aliuita uamuzi wa Mali kujiondoa kutoka kwenye kikosi cha kukabiliana na ugaidi katika eneo la Sahel Jumatano  ni jambo la kusikitisha, hasa wakati kuna ongezeko la   harakati za kigaidi na ukosefu wa usalama.

Msaidizi wa Katibu Mkuu Martha Pobee aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba uamuzi wa wiki hii wa serikali ya kijeshi ya Mali wa kuondoka kwenye kikosi hicho kwa hakika ni hatua ya kurudi nyuma kwa Sahel.

Kikosi cha G5 Sahel kiliundwa mwaka 2014 na Mali na kujumuisha mataifa jirani ya Afrika Magharibi ya Niger, Mauritania, Burkina Faso na Chad ili kukabiliana na ugaidi katika eneo la Sahel, lakini tangu mwanzo kiligubikwa na matatizo ya kifedha na kisiasa na hakikufanya kazi. Na hakikupeleka wanajeshi hadi mwaka 2017.

Hata hivyo, Pobee alisema kuwa tangu Novemba mwaka jana kikosi hicho kimefanya operesheni katika sekta zake zote tatu bila ushiriki wa vikosi vya Mali.

XS
SM
MD
LG