Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:00

Guterres amewatembelea watu waliokoseshwa makazi nchini Niger


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (C) akizungumza kwenye kambi ya Ouallam nchini Niger. May 3, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (C) akizungumza kwenye kambi ya Ouallam nchini Niger. May 3, 2022.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres siku ya Jumanne aliitembelea kambi ya watu wasiokuwa na makazi nchini Niger ambapo alihimiza misaada ya kibinadamu na kijeshi kwa nchi maskini inayopambana na waasi wanajihadi.

Guterres alisafiri hadi kambi ya Ouallam kusini-magharibi mwa nchi katika siku ya nne ya ziara yake ya Afrika magharibi iliyocheleweshwa na mzozo wa Ukraine. Alikutana na darzeni kadhaa za watu waliokoseshwa makazi na wakimbizi kutoka Niger, Mali na Burkina Faso katika uwanja wa shule uliopo kwenye kambi hiyo.

Alisema amechagua kumalizia ziara yake ya siku mbili nchini Niger pamoja na watu waliojitoa mhanga wa huko Ouallam mji uliopo mkoa wa mpakani wa Tillaberi ambao umeathiriwa vibaya na wanajihadi.

Unaweza kunitegemea kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada mkubwa kwa jeshi la Niger ili liwe na uwezo wa kuwalinda Guterres alisema. Pia alisihi kupatiwa msaada kwa watu wa Niger na wakimbizi kutoa rasilimali ambazo zilifungua njia kwa shule kwa kila mtu na hospitali zinazofanya kazi.

XS
SM
MD
LG