Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:59

Jeshi la Afrika kusini linaendelea na juhudi za kufukua vifusi na kupata maiti


Mvua kubwa zilizosababisha mafuriko eneo la KwaZulu-Natal nchini Afrika kusini
Mvua kubwa zilizosababisha mafuriko eneo la KwaZulu-Natal nchini Afrika kusini

Jeshi la Afrika kusini hadi sasa limetuma wanajeshi 400 kati ya elfu kumi waliotengwa kwa ajili ya operesheni za dharura, misaada, na ujenzi mpya katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ofisa mwandamizi wa jeshi alisema Jumatano.

Mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita ilisababisha mafuriko na maporomoko ya matope yaliyosambaa katika maeneo ya pwani ya mashariki mwa nchi na kuua zaidi ya watu 440, na kubomoa barabara, mabomba ya maji na maelfu ya nyumba. Kwa sasa tuna wanajeshi 400 kwenye eneo lakini wengine elfu kumi bado wanakuja.

Hii ni timu ya awali Brigedia jenerali Andres Mahapa aliwaambia waandishi wa habari. Timu za pamoja za kiraia na wanajeshi za kuwatafuta watu bado wanaendelea kupata maiti kutoka kwenye vifusi zaidi ya wiki moja baada ya maafa hayo kutokea. Bado tunaendelea kuchimba vifusi na kupata maiti alisema Mahapa.

XS
SM
MD
LG