Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:39

Ramaphosa anasema mafuriko ya Afrika kusini ni janga la kitaifa


Watu wakishuhudia daraja lililosomwa na maji kutokana na mafuriko huko KwaZulu-Natal nchini Afrika kusini
Watu wakishuhudia daraja lililosomwa na maji kutokana na mafuriko huko KwaZulu-Natal nchini Afrika kusini

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumatatu ametangaza kuwa mafuriko mabaya yanayolikumba taifa hilo ni janga la kitaifa, na kuonya kwamba ukarabati wa huduma za msingi utachukua muda mrefu.

Rais Ramaphosa amesema hayo katika hotuba kupitia televisheni ya taifa “Hili ni janga la kibinadamu ambalo linahitaji juhudi kubwa na za haraka za kutoa msaada. Maisha, afya na ustawi wa maelfu ya watu bado vipo hatarini” aliongeza.

Ramaphosa alisema “Bandari ya Durban ambayo ni mojawapo ya vituo vikubwa na vyenye shughuli nyingi za meli k na ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi imeathirika vibaya.”

Watu 443 walifariki, 48 hawajulikani walipo, kando na mji wa pwani ya mashariki wa Durban, rais alisema. Aliongeza kuwa bado ni tatizo kufika kwenye baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa vibaya, zikiwemo shule 16 ambazo zimeteketea kabisa.

Hali ya janga sawa na hatua zilizowekwa kupambana na janga la Covid 19 inahitaji uwezo wa kifedha wa ziada kusaidia katika ukarabati wa vilivyoharibika.

Ili kuondoa hofu kuhusu ufisadi ambao ulizorotesha juhudi za kupambana na Covid, Ramaphosa amesema serikali itaunda taasisi maalum ya uangalizi itakayojumuisha mkaguzi mkuu wa hesabu, wafanyabiashara na makundi ya kidini, pamoja na mashirika ya kitaaluma ya wahandishi na wahasibu.

XS
SM
MD
LG