Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:21

Idadi ya watu waliofariki kwa mafuriko Afrika kusini imefikia 440


Mafuriko ya KwaZulu Natal nchini Afrika kusini
Mafuriko ya KwaZulu Natal nchini Afrika kusini

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea Afrika kusini, iliongezeka hadi 440 siku ya Jumapili huku mvua ikipungua na kuruhusu shughuli za uokoaji kushika kasi baada ya moja ya dhoruba iliyosababisha vifo zaidi katika kumbukumbu za maisha.

Mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la pwani ya kusini-mashariki wikiendi iliyopita liliibua haraka mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi ambayo yaliharibu jiji la Durban na maeneo jirani yakiharibu majengo na maisha ya watu.

Kufikia Jumapili watu 443 wakiwemo wafanyakazi wawili wa polisi wa dharura walikufa kutokana na mafuriko hayo. Wanasayansi wanaona kuwa mafuriko na matukio mengine mabaya ya hali ya hewa yanazidi kuwa na nguvu na mara kwa mara kadri dunia inavyozidi kuwa na hali ya joto joto, kwa sababu mabadiliko ya hali ya hewa.

Takribani watu 63 wengine bado hawajulikani waliko na wanahofiwa kufariki baada ya mafuriko ya maji yenye nguvu sana kulikumba eneo la KwaZulu-Natal katika kumbukumbu za karibuni za kulikumba eneo hilo.

XS
SM
MD
LG