Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:57

Wanawake Mogadishu wamefungua Televisheni kuzungumzia hali zao


Mfano unaowakilisha wanawake wa Mogadishu wameamua kufungua televisheni kuelezea changamoto wanazopitia nchini Somalia
Mfano unaowakilisha wanawake wa Mogadishu wameamua kufungua televisheni kuelezea changamoto wanazopitia nchini Somalia

Kituo cha kwanza cha redio na televisheni kinachoendeshwa na wanawake nchini Somalia kimefunguliwa katika mji mkuu Mogadishu. Bilan Media inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa itatayarisha maudhui yenye lengo la kuzungumzia masuala yanayowaathiri wanawake na kutetea haki za wanawake katika nchi hiyo yenye itikadi za kiconservative.

Uzinduzi wa Bilan media mjini Mogadishu unaashiria hatua nyingine katika juhudi zinazofanywa na wanawake kupata nafasi zao katika uwanja wa umma wa mfumo dume.

Bilan inamaanisha mwangaza na wazi, kwa lugha ya Kisomali na waanzilishi wanasema watasimamia ukweli kutokana na maana hiyo kwa kuangazia baadhi ya masuala muhimu yanayowahusu na kuwaathiri wanawake.

Nasrin Mohamed Ibrahim, ni mhariri katika Bilan Media.

“Mradi huu umeundwa ili kukabiliana na changamoto nyingi zinazoikabili jamii, anasema. Italenga changamoto zinazowakabili wanawake. kuna hadithi kuhusu wanawake ambazo zitafichuliwa, kwa sababu kuna hadithi nyingi katika jamii na haziruhusiwi kuchapishwa, hivyo basi Bilan itazifichua hadithi hizo”.

Ikiendeshwa na wanawake pekee, Bilan ana matumaini ya kuvunja kizuizi katika jamii ya wenye itikadi kali nchini Somalia ambapo masuala kama vile ubakaji, unyanyasaji wa kingono na masuala ya matibabu ya wanawake mara nyingi hupuuzwa.

Bilan anasema haitafuti kushindana na vyombo vya habari vya kawaida, bali kuweka mwelekeo wake katika kuinua sauti za wanawake na kushawishi ajenda katika jamii inayotawaliwa na wanaume.

Fathi Mohamed Ahmed, ni mhariri msaidizi.

“Naweza kusema kwamba sababu ya kuanzishwa kwa chombo hiki cha habari kwa wanawake ni kwamba katika maeneo mengi ya Mogadishu na Somalia kwa ujumla, kuna vyombo vya habari ambako wote wanaume na wanawake wanafanya kazi lakini vinasimamiwa na kumilikiwa na

XS
SM
MD
LG