Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:21

Marekani yaiwekea vikwazo CRP ya Sudan


Waandamanaji nchini Sudan wakipinga mapinduzi ya jeshi ya October 2021 mjini Khartoum
Waandamanaji nchini Sudan wakipinga mapinduzi ya jeshi ya October 2021 mjini Khartoum

Watetezi wa haki za binadamu nchini Sudan wanakaribisha hatua ya wizara ya fedha Marekani ya kuweka vikwazo dhidi ya Central Reserve Police (CRP) ya nchini Sudan kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya watu wanaoandamana kwa amani.

Lakini wanaharakati hawa wanasema Marekani na mataifa mengine wanapaswa kuchukua hatua zaidi dhidi ya utawala wa kijeshi uliochukua mamlaka nchini Sudan hapo mwaka jana.

Ofisi ya idara ya fedha marekani ya udhibiti wa Mali za kigeni (OFAC) ilitangaza Jumatatu kwamba mali na maslahi yote ya CRP zilizoko ndani au zinazoingia Marekani, au ambazo zinamilikiwa, au kudhibitiwa na watu wa marekani zimezuiliwa na lazima ziripotiwe kwa OFAC. Mohamed Osman, mtafiti wa Human Rights Watch alisema CRP imekuwa ikishutumiwa kwa kuwakandamiza waandamanaji wa Sudan tangu mapinduzi ya Oktoba 25. Alibainisha kuwa kitengo cha polisi kina rekodi iliyothibitishwa ya unyanyasaji wakati wa maandamano ya mwaka 2018 na 2019 ambayo yalipelekea kuondolewa madarakani kwa Rais wa muda mrefu nchini Sudan, Omar al-Bashir na kabla ya hapo katika maeneo yenye migogoro ya Darfur na Kordofan.

XS
SM
MD
LG