Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 21:20

Uingereza itatoa dola milioni 100 kwa Ukraine


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Uingereza itatoa dola milioni 100 kwa Ukraine kupitia benki ya dunia kwa lengo la kudumisha utendaji kazi wa serikali na kupunguza shinikizo la kifedha lililosababishwa na uvamizi wa Russia, ofisi ya waziri mkuu Boris Johnson ilisema.

Uingereza inatafuta jukumu kuu katika majibu ya kimataifa kwa uvamizi wa Russia kwa Ukraine kwa kutoa msaada wa kijeshi wa kujitetea ikitaka kuwepo tena vikwazo vikali kwa Kremlin na kutoa msaada wa kifedha.

Hata hivyo serikali ya Johnson inakabiliwa na ukosoaji kwamba vikwazo vyake vimekuwa polepole mno na program yake ya wakimbizi ni dhaifu. Duru ya hivi karibuni ya fedha taslim, ambazo ni ziada ya dola milioni 290.95 tayari ziliahidiwa zinaweza kutumika kuwalipa wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Ukraine au malipo ya uzeeni na mafao mengine, mamlaka ya Uingereza ilisema.

“Ingawa ni Putin pekee anayeweza kumaliza madhila haya nchini Ukraine, ufadhili mpya wa fedha wa leo utaendelea kuwasaidia wale wanaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu”, Johnson aliongeza.

Fedha hizo zitatolewa kupitia World Bank Multi-Donor Trust Fund, ambao umeundwa ili kuharakisha ufadhili kwa Ukraine na tayari unatumiwa na baadhi ya mataifa mengine.

XS
SM
MD
LG