Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:15

Tanzania yasisitiza kuzidisha ushirikiano DRC


Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akipokea maelezo katika kambi ya MONUSCO Beni
Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akipokea maelezo katika kambi ya MONUSCO Beni

Waziri wa ulinzi wa Tanzania, Hussein Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazo shiriki katika kuleta amani mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mwinyi alitoa wito huo siku ya Ijuma alipowatembelea wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la Disemba 7, 2017.

Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuwawa na wengine 44 kujeruhiwa walipo shambuliwa na waasi wasiojulikana hadi hii leo katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.

Waziri wa ulinzi wa Tanzania Mwinyi azungumza akiwa Beni
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:43 0:00

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Beni, Waziri Mwinyi alisema amefika kuwapa pole wanajeshi wa Tanzania na kuwatembelea walojeruhiwa pamoja na kuwapa moyo kuendelea na jukumu lao la kurudisha amani katika eneo la mashariki ya Kongo.

Akizungumzia uchunguzi unaoendelea kuhusu shamblizi hilo, Mwinyi amesema hadi sasa hawana habari zaidi, "sasa hivi ni mapema sana kusema fulani amefanya hivi. Hatuna uhakika, UN pia haina uhakika na ndiyo maana tunasema ni lazima uchunguzi ufanyike."

Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akiwasalimia wanajeshi wa Tanzania mjini Beni DRC
Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akiwasalimia wanajeshi wa Tanzania mjini Beni DRC

Anasema uchugunzi ukifanyika utawawezesha kujipanga vyema zaidi ili tukio kama hili lisitendeke tena au likitendeka wawe tayari kukabiliana nalo, akitoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya pande zote zinazohusika na shughuli za kulinda na kurudisha amani mashariki ya Kongo.

XS
SM
MD
LG