Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:55

Trump aamrisha mashambulizi dhidi ya Syria


Manuari ya jeshi la majini la Marekani USS Ross ikifyetua kombora la Tomahawk kuelekea Syria Ijuma 7, 2017
Manuari ya jeshi la majini la Marekani USS Ross ikifyetua kombora la Tomahawk kuelekea Syria Ijuma 7, 2017

Akilihutubia taifa kutoka nyumbani kwake huko Mar-a-lago, Florida Alhamisi usiku, rais Trump, alisema "hii leo nimeamrisha shambulio la kijeshi kulenga uwanja wa ndege wa Syria ambao ulitumiwa kufanya shambulizi la kemikali siku ya Jumanne."

Kombora la aina ya Tomahawk likifyetuliwa dhidi ya Syria
Kombora la aina ya Tomahawk likifyetuliwa dhidi ya Syria

Katika hotuba yake ya dakika tatu, kiongozi wa Marekani anasema, kiongozi wa kimabavu wa Syria, Bashar al-Assad alifanya shambulizi la kikemikali la kikatili dhidi ya raia wasio na hatia.

"Hakuna shaka yeyote kwamba Syria ilitumia silaha za kemikali zilizopigwa marufuku, ikikuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Silaha za Kemikali, na kupuuzi wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa", alisema Rais Trump.

Rais Donald Trump akizungumza kutoka Mar-a-Lago huko Palm Beach, Florida, April 6, 2017.
Rais Donald Trump akizungumza kutoka Mar-a-Lago huko Palm Beach, Florida, April 6, 2017.

Afisa wa jeshi la Marekani ameiambia Sauti ya Amerika kwamba manwari za kijeshi za Marekani USS Porter na USS Ross zilifyetua makombota 59 ya aina ya Tomahawk, kutoka Bahari ya Mediterranean hadi kambi ya jeshi la anga la Syria karibu na mji mkuu wa Damuscus.

Shambulio hilo lilifanyika wakati Trump alikua katika chakula cha usiku na Rais Xi Jingping wa China aliyewasili Marekani hii leo kwa mazungumzo ya siku mbili.

Trump alisema Marekani ililazimika kuchukua hatua hiyo kwa maslahi yake ya kitaifa ili kuzuia kusamba kwa silaha za hatari za kemikali.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kufikia makubaliano juu ya mswada wa azimio la kulaani shambulio la kemikali karibu na mbi wa Idlib lililofanywa na serikali ya Damuscus.

XS
SM
MD
LG