Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:12

Uganda yashindwa kuwika dhidi ya Ghana


Wachezaji wa Uganda wakijaribu kupokonya mpira kutoka Ghana
Wachezaji wa Uganda wakijaribu kupokonya mpira kutoka Ghana

Uganda Cranes walijitahidi katika mchuano wao wa kwanza katika finali za Kombe la Afrika baada ya miaka 39, waliposhindwa bao moja kwa bila na Black Stars wa Ghana.

Andre Ayew, aliwapatia Ghana lao pekee katika dakika 32 ya nusu ya kwanza ya mchezo pale Isaac Insinde kufanya dhambi katika eneo tete na kusababisha mkwaju wa penelty.

Tangu wakati huo Ghana ilionekana kutotafuta bao jingine bali waliweka ngome kali ambayo waganda hawakuweza kupenya. Hivyo Blak Stars kujipatia ushindi wao muhimu wakiwa na nia ya kurudi nyumbani na kombe safari hii baada ya kushindwa mara ya mwisho na mabingwa Ivory Coast huko Equatorial Guinea 2015.

Uganda ambao wanarudi kwa mara ya kwanza katika finali za Kombe la Afrika tangu 1978 wanamatumaini ya kufika mbali katika michuano hiyo.

XS
SM
MD
LG