Wagombea kiti cha rais wa Marekani wanakamilisha kampeni zao za uchaguzi wa kipekee kwa kufanya mikutano ya saa sita za usiku saa chache kabla ya watu kuanza rasmi kupiga kura. Donald Trump mgombea wa chama cha Republican akiwa na umati mkubwa wa watu anaendelea kusema hana haja ya wasani wakuu kuwavutia wapigaji kura.
Anasema hawamhitaji Byonce, wala Lady Gaga, Jay Z au wengine. Mgombea huyo ametembelea majimbo matano mnamo siku moja ili kuwahamaishsha wapiga kura na alipofika North Carolina alisma imebaki siku moja pekee yake.
"Katika muda wa siku moja tu, unaweza kuamini, Siku moja tu iliyobaki tutashinda jimbo muhimu la North Carolina na tutaichukua tena White House. Uchaguzi huu utamua ikiwa tutatawaliwa na kundi la wanasaiasa walaji rushwa mumeshuhudia yaliyokua yakitendeka. Au ikiwa tutatawaliwa na wananchi . tutatawaliwa na wananchi bila shaka".
Trump anajivunia kwamba ana mikutano mikubwa zaidi kuliko mpinzani wake Clinton ambae pia siku ya mwisho ametembelea majimbo matano yenye ushindani.
Na katika jimbo la Philadelphia ambalo linaonekana linaelekea upande wa wake alitoa vigogo wake wote kuanzia muimbaji mashuhuri Bruce Springstien , rais Barack Obama, mkewe Michele na wakuu wa chama.
Obama amewataka wapigaji kura kujitokeza kwa wingi.
"Sasa, ninafahamu imekua kampeni ndefu kweli kweli. Kumekua na makelele chungu nzima vituko mbali mbali hata utafikiri ni mchezo wa kuchekesha. Lakini kesho Kesho waphiladelphia uwamuzi uko mikononi mwenu ukingia katika kituo cha kupiga kura chaguo ni wazi kabisa mbele yenu".
Akihutubia mkutano mkubwa kabisa wa kampeni yake ulokua na karibu watu elfu 33, Bi. Clinton amesema,
"Chaguo katika uchaguzi huu ni wazi kabisa kati ya kutengana au kuungana kati ya uchumi unaofanya kazi kwa watu wote au kwa wale tu wa juu, kati ya uwongozi thabiti au ule usiotabirika utakao tuweka hatarini"
Uchunguzi wa maoni ulotolewa siku ya mwisho ya kampeni na vyuo vikuu mbali mbali na mashirika ya habari yanampatia ushindi mdogo Hillary Clinton upande wa kura za wananchi, lakini nafasi kubwa zaidi katika wajumbe wa Jopo la Uchaguzi.