Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:40

Jopo la AU laitaka Kenya kufanya mageuzi katika sheria za uchaguzi


Karani wa uchaguzi wa Kenya akikusanya ripoti kutoka sanduku za kura.
Karani wa uchaguzi wa Kenya akikusanya ripoti kutoka sanduku za kura.

Jopo la wafuatiliaji la Umoja wa Afrika, AU, limetoa wito wa kufanyika kwa haraka mageuzi ya sheria na utaratibu wa uchaguzi na mahakama huko Kenya ili kuepusha mzozo sawa na ulozukawakati wa uchaguzi mkuuwa 2007.

Hati ya ripoti ambayo VOA iliweza kupata iliyotayarishwa na wafuatiliaji wawili waloteuliwa na AU itatoa shinikizo kwa wanasiasa wa juu hasa wale wa serikali, kuanzisha mazungumzo na wadau wote ili kukubaliana juu ya mpango mpya kuelekea uchaguzi.

Miongoni mwa mambo ndani ya ripoti hiyo iliyotolewa kwa siri inaeleza kwamba upinzani kujtokua na uwaminifu na tume ya uchaguzi na hali ya kutoelewana juu ya hatima ya majaji wa Mahakama Kuu, huwenda kukasababisha kutokea kwa ghasia kabla ya uchaguzi.

Wapinzani wakizusha ghasia baada ya uchaguzi wa August 2017.
Wapinzani wakizusha ghasia baada ya uchaguzi wa August 2017.

Ripoti inatoa wito wa kuwepo mazungumzo ya dhati kati ya vyama mbali mbali, hata hivyo ripoti haikutoa wito wa kufanywa mabadiliko jumla katika tume ya uchaguzi kama vile upinzani wa Kenya unavyodai.

XS
SM
MD
LG