Kura mpya ya maoni inaonyesha seneta Bernie Sanders na Bilionea na mfanyabiasha wa nyumba Donald Trump bado wanaongoza kwa kiasi kikubwa katika kura hizo kwenye jimbo la New Hampshire.
Kura ya maoni iliyotolewa na Chuo kikuu cha Monmouth ulionyesha Trump akiongoza kwa asilimia 30 kwa wapiga kura watarajiwa wa chama cha Republikan katika jimbo hilo haijabadilika kutoka mwezi mmoja uliopita.
Trump anaongoza kwa alama 16 mbele ya mpinzani wake wa karibu Gavana wa Ohio John Kasich ambaye anashindana vikali katika nafasi ya pili na Seneta wa Florida Marco Rubio, seneta wa Texas Ted Cruz na gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush.
Kwa upande wa wademokrat unaonyesha Sanders akiwa anaongoza kwa alama 10 dhidi ya waziri wa mambo ya nje wa zamani Hillary Clinton . Ikiwa zimepungua kutoka alama 14 mwezi uliopita.